Talisman Brisé ni tamthilia ya redio inayosimulia hadithi ya mtunza bustani Kwame ambaye bosi wake Profesa Omar anatekwa nyara na watu wasiojulikana. Kwa nini Profesa Omar anatekwa nyara na watu hao? Mfanyakazi wake Kwame atafanikiwa kumuokoa Bosi wake? Fuatilia haya kwenye tamthilia ya Talisman Brise hapa rfi kila siku ya jumapili ndani ya Makala ya Changu Chako Chako Changu.